Ibadhi.com

09. SEMA IMEKUJA HAKI - UKAFIRI,VIGAWANYO VYAKE NA UOMBEZI

UKAFIRI,VIGAWANYO VYAKE NA UOMBEZI

MWANAFUNZI:  Sheikh wangu, nimesikia kwa baadhi ya watu wa makundi mengine wakiwatuhumu Ibadhi kuwakufurisha wengine, naomba unibainishie neno la ukafiri na vigawanyo vyake kwetu sisi kama vipo.
SHEIKH:  Ewe mwenye kutaka uongozaji, mwenye kiu ya kujua haki, nakuletea uhakika, nao ni kuwa Ibadhi wameugawa ukafiri sehemu mbili: Ukafiri wa kishirikina na Ukafiri wa neema, Na vigawanyo hivyo vyote mafikio yake ni mabaya.
MWANAFUNZI: Umetaja sheikh wangu neno UKAFIRI WA NEEMA, ni nini maana yake ? na unatofautiana vipi na ukafiri wa kishirikina ?
SHEIKH: Wewe ni mwanafunzi hodari, Allah mtukufu akubariki, jua ukafiri wa neema sio ukafiri wa kishirikina, neno hilo hutumika kwa kila mwenye kufanya madhambi makubwa au akaacha yale aliyomuwajibishia Allah mtukufu, nao ni Ukafiri haumtoi katika mila ya uislamu, hukmu zake ni kama hukmu za waislam wengine, Maibadhi wanahesabu kuwa mwenye kufanya dhambi kubwa ni kafiri wa neema. Haijuzu kumwita Muumin na inawajibika kumchukia kwa ajili ya Allah mtukufu.
MWANAFUNZI: Allah mtukufu atukinge na maasi, na atuzidishie kupenda utiifu wake, Allah mtukufu akujazi kheri ewe sheikh wetu, kama naona katika macho yako kuna ziyada unataka kunipa nimiminie ewe sheikh wangu.
MWALIMU: ndio ewe mwanangu, nilitaka uzinduke katika vitundu vidogo viwili:

1. Yapo makosa yamekuwa makubwa katika jamii yetu, na yote yanaingia katika ukafiri wa neema, katika hayo ni kutokutoa zaka, kula riba, uzinifu n.k.
2. Ukafiri wa neema unafahamka katika qur-an kwa jina hilo la ukafiri na majina mengine kama ufaasiq, faajiri, maasi, dhulma, unaafiq, kabiirah, hivyo uzinduke usomapo Qur-an ii ujue mafikio ya kundi hili, na uhakika ni kuwa kundi hili la makafiri wa neema wamesilimu kwa matamko tu sio kwa vitendo, ubaya ulioje wa uovu wao!

MWANAFUNZI: Shukrani ni za Allah mtukufu aliyetuongoza katika usawa, tusingeongoka kama si kutuongoza kwake Allah mtukufu, … Sheikh wangu niambie kuhusu mwenye kufanya madhambi makubwa, hivi atapata uombezi siku ya qiyama hali ya kuwa Allah mtukufu anasema: (( Wala hawamwombei yeyote ila yule anaye mridhia Yeye…)) Anbiyaa:28
SHEIKH: Ni swali muhimu sana ewe mwanangu; Mwenye kufanya madhambi makubwa ni kafiri ukafiri wa neema, hatopata uombezi siku ya Qiyama, na vipi atapata shafaa aliyekufa naye anamuasi Allah mtukufu, Allah mtukufu anasema: )) Madhaalimu hawatakuwa na rafiki, wala mwombezi wa kuitikiwa.)) Ghaafir :28
Na law ingekua uombezi ni kwa wafanyao madhambi makubwa basi ingekuwa watu wanajikurubisha kwa Allah mtukufu kwa madhambi..!!!, na kwaajili hiyo wameshuhudia wasiokuwa katika madhehebu yetu kuwa itikadi yetu ndiyo ya sawa, amesema Sheikh Abdul muizz Abdusattar: “Law Ummah ungechukua itikadi yenu katika kubakia milele katika adhabu kwa mfanya madhambi makubwa, ingekuwa ummah huu una sehemu kubwa ya wema, msimamo, usafi na heshima tofauti na tunavyoona leo”
MWANAFUNZI: Subhaanallah!! Inanidhihirikia kuwa baadhi ya pande za madhehebu wameweka tafsiri vibaya pamoja na kuwepo kwa dalili za wazi kuwa Uombezi wa Mtume –Sallallahu alayh wasallam- ni kwa wachamungu tu, nayo ni kwa kuwazidishia daraja za pepo.
SHEIKH: Allah mtukufu akubarik ewe mwanangu, Je unaijua hukmu ya Qur-an kwa wenye kufanya madhambi makubwa ?
Endelea na jawabu katika makala ifuatayo….

Khamis bin Yahya bin Khamis Alghammawi

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.


Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment