Ibadhi.com

8.SEMA IMEKUJA HAKI - KUMCHUKIA MWENYE DHAMBI KUBWA

 

KUMCHUKIA MWENYE DHAMBI KUBWA


MWANAFUNZI: Allah kuzidishie malipo ewe Mwalimu wangu, naomba turejee kuhusu mwenye madhambi makubwa, vipi inatustahikia kumchukia ?
SHEIKH: Allah akubarik ewe mwanafunzi mwenye Himma, ili ufahamu hilo wacha nikuwekee wazi nukta muhimu kwetu sisi Ibadhi, nayo ni kuwa wanachuoni wetu wamegawa WALAAYA sehemu tatu:
SEHEMU YA KWANZA: WALAYA YA JUMLA: nayo ni kuwapenda waumini na wanawake waumini tangu kuumbwa kwa Adam mpaka kitakaposimama Qiyama, katika binadamu, majini na malaika.
SEHEMU YA PILI: WALAYA YA UHAKIKA: nayo ni kuwapenda wote waliotajwa na Allah mtukufu kuwa ni waliofaulu kupata Pepo, sawa ikiwa ni katika Qur –an au Hadithi Mutawaatir
SEHEMU YA TATU: WALAYAT ASHKHAAS: nayo ni kuhukumu kwa mujibu wa dhaahir kwa kila atakayejilazimisha kufuata amri ya Allah mtukufu na kuacha makatazo yake, wala hakubakia katika dhambi ndogo na hafanyi dhambi kubwa ispokuwa ataiombea toba.
Na hivyo hivyo BARAA inagawika katika sehemu hizo tatu (( Jumla, Uhakika, na Ashkhaas)) na hapa kuwachukia watu waovu kunaingia katika Baraa ya Ashkhaas, na ili ujue sababu basi jiulize ni ipi hoja ya kusimama Baraa kwa pamoja ? Utajibu: Sababu ni kutotekeleza sehemu katika amri za Allah mtukufu au kufanya chochote katika makatazo yake
Basi nitakwambia: kwa hivyo sababu ya kuwajibika baraa kwa jumla ipo kwa huyo mfanya mfanya madhambi makubwa, hivuo imetuwajibikia kupitisha hukmu ambayo imewajibika kwa sababu hiyo, ikathibiti hukmu hiyo kwa kipimo hiki moja kwa moja, na ukitaka jizidishie Yaqini kwa kauli ya Allah mtukufu: "Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yaliyo mchukiza Allah mtukufu na wakachukia yanayo mridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao” Muhammad:28 Na hapana budi kuzingatia mambo mawili:
JAMBO LA KWANZA: Kuwachukia wenye madhambi makubwa haimaanishi kumtoa katika mila ya uislamu, bali atabaki katika safu za waislamu, atapata wanachopata na anawajibika na yanayowajibika ispokuwa kuchukiwa moyoni, na atanasihiwa ili kubadilisha uovu wake, akitubia toba ya kweli hubadilika na kuwekwa katika WALAAYA.
JAMBO LA PILI: Aliyomo katika Baraa hahukumiwikuwa ni mtu wa motoni, Baraa ni hukmu ya kidunia, amma ghaibu ni ya mjuzi wa ghaibu, hivyo jua kuwa hukmu hizi ni kwa mujibu wa dhahiri kwa kuangalia Qauli na vitendo, mfano: Mwizi, Mzinifu, mlevi wa pombe, myoa ndevu, na mwenye kuburura nguo zake, na kila mwenye kubakia katika dhambi ndogo, kwa kuwa hakunadhambi ndogo pamoja na kubakia nayo, hivyo jua inakuwajibikia kuwachukia, amesema Allah mtukufu: "Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao." Maidah : 51
MWANAFUNZI: Itie nuru akili yangu ewe Mwalim wangu, ni ipi athari ya itikadi ya Walaaya na Baraa ?
SHEIKH: Swali hili ni Muhimu sana, kwa kulijua jawabu yake nafsi yako itachangamka na itanyanyuka himma yako ili uitekeleze itikadi hii katika uhalisia kama walivyofanya wema waliokutangulia, kwa kuwa walifuata amri ya mola wao ikaleta itikadi hiyo matunda mema, na katika faida hizo ni zifuatazo:


Khamis bin Yahya Alghammawi

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Ibadhi.com

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment