Ibadhi.com

06. SEMA IMEKUJA HAKI - WALAYA NA BARAA

 


WALAYA NA BARAA


MWANAFUNZI: Imeonekana asubuhi kwa kila mwenye macho mawili, akili yangu imejua mengi katika yanayowaijibikia kuhusu Allah mtukufu katika kumtakasa na kila upungufu. Wema wako ulioje ewe sheikh wangu na muongozaji wangu katika kheri, lakini umebaki moyo wangu unataka kujua kuhusu hukmu uloitaja huko nyuma, nayo ni Walaaya na Baraa, naomba unipe funguo zake.


SHEIKH: Ukubwa ulioje wa jitihada yako katika kutafuta ilmu, na ni kheri kubwa kufanya jitihada ya kumungoza mwanafunzi hodari kama wewe, Allah mtukufu akuelimishe, Jua kuwa katika wajibu wa mukallaf baada ya tauhidi ya kumpwekesha Allah mtukufu ni kumpenda mwema kwa wema wake (( walaaya)) na kumchukia muovu kwa uovu wake (( baraa)) na vyote hivyo ni faridha za kidini, Amesema Allah mtukufu “ Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi" taubah:71 na imepokewa kutoka kwa Mtume S.A.W. “Nguzo yenye nguvu zaidi katika uislamu ni kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allah mtukufu” Ahmad : 18547


MWANAFUNZI: Niwekee wazi – mwalimu wangu – makundi ya watu kwa mujibu wa walaaya na Baraa.


SHEIKH.  Katika madhehebu ya Ahlil haqq wal Istiqaama, watu kwa mujibu wa kujilazimisha kwao na sharia wapo makundi matatu, niazime ufahamu wako :
· KUNDI LA KWANZA: Wanaojulikana wema wao, hao ndio wapo katika WALAYA.
· KUNDI LA PILI: Wanaojulikana kwa uovu au kutojilazimisha katika wajibu, hao wapo katika BARAA.
· KUNDI LA TATU: Wasiojulikana wema wao na ubaya wao, hao wapo katika WUQUUF.


Na upambanuzi wake ni kama ifuatavyo:
WALAAYA: Ni kupenda kwa moyo, kusifu kwa ulimi, kuwanusuru, kuwasaidia, na ulazima wa kuwaombea rehma na msamaha kwa waumini, Amesema Allah mtukufu: "Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi " Tauba : 71 BARAA: Ni kuwachukia na kutojuzu kuwaombea rehma na msamaha kwa mwenye kuchukiwa, kwa kauli yake Allah mtukufu: "Enyi mlio amini! Msiwafanye rafiki zenu watu ambao Allah mtukufu amewakasirikia." Mumtahina: 13, WUQUUF: Nayo ni kujizuia kutoa hukmu ya kupenda au kuchukia kwa kukosekana dalili ya yaqini ya wema au uovu wake, kwa qauli ya Allah mtukufu: " Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo” Israa:36 Na amesema Mtume s.a.w. “Na ikiwa jambo lina utata, basi simama – usilitolee hukmu yoyote-”


MWANAFUNZI: Allah mtukufu akuzidishie malipo ewe Mwalimu wangu, naomba turejee kuhusu mwenye madhambi makubwa, vipi inatustahikia kumchukia ? …………………………………..

Khamis bin Yahya Alghammawi Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona. https://ibadhi.com

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment