Ibadhi.com

05.SEMA IMEKUJA HAKI - KUUMBWA KWA QUR-AN

KUUMBWA KWA QUR-AN

Sheikh: Je wakusudia mas ala ya kuumbwa Qur an?
Mwanafunzi: Ndio, hayo ndiyo nliokusudia
Sheikh: Je waamini kuwa kila asiyekuwa Allah mtukufu ni kiumbe ?
Mwanafunzi: Hakuna shaka katika hilo, kwani Allah mtukufu ndio muumbaji wa kila kitu.
Sheikh: Basi hilo linakutosha kujua kuwa Qur an ni kiumbe, na siyo kama yasemavyo baadhi ya makundi ya kwamba ni ya tangu, ilikuwepo tangu zamani.
Mwanafunzi: Hivi hili ndilo wanalozozana kwalo,? Nizidishie dalili sheikh za wasemao Qur an ni kiumbe
Sheikh: Wametoa dalili nyingi, katika hizo ni aya kumi na nne kutoka katika Qur an pekee, ukiongezea dalili katika sunnah na dalili za kiakili, na katika dalili zao:
Qur an imekuwepo baada ya kutokuwepo, athari za utengenezaji zipo wazi juu yake, kwani herufi moja inahitajia herufi nyingine ili liwe neno, na kila neno linahitajia neno lingine ili iwe sentesi.
Pia Qur an ipo katika vifua, na katika ubao uliohifadhIwa, na kinachokuwa katika kiumbe pia na chenyewe ni kiumbe
Pia Qur an imetokezeshwa, kama asemavyo Allah mtukufu: " Hayawafikilii mawaidha yaliyotokezeshwa kutoka kwa Mola wao Mlezi ila huyasikiliza na huku wanafanya mchezo” Anbiyaa:2 pia Qauli ya Allah mtukufu “Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman ila wao hujitenga nao” Ashuaraa:5


Na kutokezeshwa ni kufanywa kuwepo baada ya kutokuwepo.

Na dalili kama nilivyokwambia ewe mwanangu ni nyingi na za wazi hazijifichi kwa kila mwenye akili, na kwa kuwa ninajua una shauqu ya ilmu, nakuusia kusoma kitabu Alhaqq Daamigh na kitabu “ Albuud alhadwaari lil aqiidatil ibadiyya” na kitabu “Bahjatul anwaar sharh anwaarul uquul” huko utapata ukitakacho, yatakayoondosha kiu yako katika masuala uloyaleta.

Mwanafunzi: Imeonekana asubuhi kwa kila mwenye macho mawili, akili yangu imejua mengi katika yanayowaijibikia kuhusu Allah mtukufu katika kumtakasa na kila upungufu. Wema wako ulioje ewe sheikh wangu, na muongozaji wangu katika kheri, lakini umebaki moyo wangu unataka kujua kuhusu hukmu uloitaja huko nyuma, nayo ni Baraa, naomba unipe funguo zake.


Khamis Yahya Alghammawi Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona. ibadhi.com

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment