Ibadhi.com

04. SEMA IMEKUJA HAKI - KUTAZAMA SIO KUONA


KUTAZAMA SIO KUONA


Mwanafunzi: Lakini kutazama hapa kunaweza kuwa na maana nyingine au sivyo ewe sheikh wangu ?


Sheikh: Ahsant ewe mwanangu, hakika kutazama kwa waarabu kuna maana nne hakuna ya tano yake, nayo ni :


1. Huruma na rehema
2. Kuzingatia
3. Kungojea
4. Kuona kwa jicho


Na zipo aya nyingi katika Qur an katika maana hizi, basi kutazama hapa maana yake ni kungojea sio kuona kwa jicho, kwani hilo ndilo linalokubaliana ushahidi wa kiakili na mfuatano wa aya, kwani Allah mtukufu ametaja makundi mawili: Kundi la wema lenye furaha likingojea rehma za mola wao mlezi na kundi la waovu likingojea adhabu kali zenye kuumiza. Na haya ndiyo aliyotaja Allah katika surat Abasa aliposema “Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri, Zitacheka, zitachangamka, Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi, Giza totoro litazifunika, Hao ndio makafiri watenda maovu” 38 – 42, na ukitaka ziada basi kasome kitabu cha Burhaanul haqq cha Samaahat Sheikh Ahmed Alkhalili – Allah amuhifadhi -, huko dalili zimepambanuliwa zaidi.

Mwanafunzi: Subhaanallah…! Hivi baada ya hoja hizi, bado kuna watu wanaamini kuwa Allah mtukufu ataonekana.

Sheikh: Usishangae, Bali kuna wengine wamejuzisha Allah mtukufu kuonekana duniani pia, na wale walojuzisha kuonekana Akhera wametofautiana kuhusu nani atakayemuona katika waja wake, je ni waumini peke yao au ni waumini na wanafiqi au watu wote hata washirikina? Je ni wanaume peke yao au hata wanawake pia ?, Je watamuona katika kisimamo cha qiyama au peponi ?, hivi tofauti hizi zinaendana na itikadi, kauli zao zimegongana kwa mgongano wa dalili zao, kwani wanadai kuwa hadithi ya Abi Hurairah inathibitisha kumuona katika kisimamo, wakati hadithi ya Suhaib yathibitisha peponi !! Wakati hadithi ya Abi Huraira inawathibitishia wanafiki na waumini, hadithi ya Suhaib inawataja waumini tu.

Mwanafunzi: Umebainisha na kuongoza ewe sheikh wangu, umeweka wazi na kutosheleza, Allah mtukufu akulipe kutokana nasi malipo awalipayo waja wake waongozaji, nimebaki nina swali kuhusu fitna iliyotokea zama za ukhalifa wa Bani Umayya, na akafungwa kwa sababu hiyo Imaam Ahmad bin Hambal ?

Mwalimu : Je wakusudia mas ala ya kuumbwa Qur an? …. Endelea nasi wiki ijayo.


Khamis Yahya Alghammawi Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona. ibadhi.com

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment