Ibadhi.com

02.SEMA IMEKUJA HAKI - SIFA ZA ALLAH MTUKUFU


SIFA ZA ALLAH MTUKUFU


Mwanafunzi: Kwa haki, nimekuwa muhitaji kwako na uongozi wako ewe sheikh wangu, nikitamani maelekezo yako, basi niongoze katika uhakika wa sifa za Allah mtukufu.

Sheikh: - Jua ewe mwanafunzi mwenye akili- kuwa sifa za Allah mtukufu ni za tangu, nazo ndiyo yeye mwenyewe Allah mtukufu, wakati huo huo Asha’ariyya wanaona kuwa sifa za Allah mtukufu ni maana hakika zilizozidi katika dhati yake, na dhati yake imesimama kwa sifa hizo.

Mwanafunzi: Ni ipi hoja yetu katika hilo ?

Sheikh: Ewe mwanangu nipe fikra yako – Allah akuangazie kwa ilmu uoni wako – “Lau zingekuwa sifa za dhati za Allah mtukufu si yeye mwenyewe, italazimu kuwa imam ziwe zimeingia ndani ya dhati yake nalo bila shaka ni batili kwa kuwa Allah mtuku si sehemu ya kuingiwa na vitu, amma ziwe sifa hizo ni sehemu ya dhati yake, nayo ni batili kwa kuwa dhati ya Allah mtukufu haigawiki, na kugawika kwake ni jambo lisilowezekana, amma sifa hizo ziwe ni ziada katika dhati ya Allah mtukufu, nalo ni batili kwa kuwa italazimika kwa Allah mtukufu kuhitajia hiyo ziada, Nay Allah mtukufu si muhitaji na kila muhitaji si Mola mwenye kustahiki kuabudiwa, kwa kuwa hajiwezi mwenyewe, anategemea kwa vitu vingine”
Pia ikiwa sifa za dhati si yeye mwenyewe Allah mtukufu imma zilikuwa pamoja na Allah mtukufu tangu azali, na hii italazimika kuwa na waliotangulia wengi, nayo ni batili 100%, au ziwe sifa hizo zimemtangulia Allah mtukufu kwa hivyo italazimika kuwa Allah ametokezea baada ya sifa zake, nayo ni batili bila shaka yoyote, kwa kuwa Allah mtukufu hana mwanzo na hakuna aliyemtangulia. Imma ziwe sifa za Allah mtukufu zimekuja baada ya Allah mtukufu nayo ni batili bila shaka kwa kuwa italazimika kuwa Allah alikuwepo bila sifa zake, yaani hakuwa na ilmu, uhai,uwezo n.k na hivyo kuzihitajia sifa hizo. Na hapa inathibiti tunayosema – kuwa sifa zake ni yeye mwenyewe – na yanabatilika wayasemayo wengine”

Mwanafunzi: Namshukuru Allah mtukufu aliyenionyesha njia ya uhakika, Allah mtukufu akuongezee fadhila ewe sheikh wangu… Nimesikia baadhi ya watu wanamuomba Allah wakisema “Mola niruzuku ladha ya kutazama uso wako mtukufu”, Sheikh wangu niwekee wazi qauli hizi – Allah asininyime elimu yako – hivi kweli waja watamuona mola wao ?

 

-----------------------------------------------------------------------------

[1] - Alsaalimi Abdullah bin Humeid: Bahjatul Anwaar Sharh Anwaaril uquul fii tauhiid, chapa 4, Maktabat Imaam Saalimi, Siib 2003m uk 80

 

Khamis bin Yahya Alghammawi    

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.  

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment