Ibadhi.com

1.SEMA IMEKUJA HAKI - UTANGULIZI

Kwa jina la Allah mtukufu, muongozaji katika haki, mwenye kusema kumwambia mwanadam “ Hakika sisi tumemuongoza njia, Imma awe mwenye kushukuru au awe mwenye kukufuru”, Rehma na Amani zimwendee Mtume Muhammad s.a.w. Yule aliyetuwekea wazi kuwa wenye kumfuata yeye, hao ndio “kundi la peponi” na kwamba watakaomuasi yeyem, hao ndio “kundi la motoni”, Baada ya hayo:-
Jua – ewe mwenye kutaka uongofu – kuwa itikadi sahihi ndio muelekezaji katika tabia njema na fikra ilosalimika, na ndiyo siri ya furaha ya mwanandamu katika maisha haya ya dunia, kama ambavyo ndiyo sababu na msingi wa kuthibiti kwa muumin katika njia iliyonyooka yenye kufikisha katika pepo yenye neema. Na kwa ule umuhimu mkubwa wa ITIKADI ilikuwa yatakiwa ewe muislam uipe umuhimu kupindukia, kwa kutafuta elimu.
Kwani matamanio mengi ya watu na shubha mbovu vimechanganywa katika Itikadi, basi ni vizuri kwako ewe mwanafunzi wa elimu uisafishe itikadi yako kutokana na uchafu huo, kwa kuifuata haki katika mambo yote ya kiitikadi. Ukishikamana na kitabu cha Allah mtukufu, ukijiongoza kwa Sunnah toharifu ya Mtume s.a.w., Ukiachana na ung’ang’anizi mbaya, na kufuata mkumbo wa upofu.
Itikadi ni Yaqini anayoamini mtu kwa mola wake, sio ufuasi wa waliotangulia au wanachuoni bila ya kutafuta dalili ya wazi, muumini anachukua dini yake kwa nguvu, na nguvu haiwi katika kuiga bali kushikana na hoja zilizo wazi, bainifu.
Ewe ambaye utakwenda nami katika mfululizo huu, fikiri vizuri, na shughulisha akili yako, na himiza khatua zako ili uwe katika safari yetu ya WALIO ONGOKA, kupitia maswali ya mwanafunzi mwenye akili kwa Shekh wake, hizi ni nuru zing’arishazo njia yako, basi “Simama imara kama ulivyoamrishwa”.
Mwanafunzi: Kwa haki, nimekuwa muhitaji kwako na uongozi wako ewe sheikh wangu, nikitamani maelekezo yako, basi niongoze katika uhakika wa sifa za Allah mtukufu….


Mwalimu :…. Endelea nami katika makala ya pili

 

Soma Makala Yaliopita - Safina Ya Uongofu.

 

Khamis Yahya Alghammawi      

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.             

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment