Ibadhi.com

31. DUA ANAPOPATWA NA MACHUNGU YA MOYO, NA HUZUNI

I. Kasema Abdillahi R.A.A., "Kasema Mtume S.A.W., "Haimpati yeyote yule chembe ya masikitiko, na wala huzuni akasema,[1] " (ikiwa anaeomba na mwanamume).

اللَّهُمَّ إِنِّي عَبْدُكَ وَابْنُ عَبْدِكَ وَابْنُ أَمَتِكَ نَاصِيَتِي بِيَدِكَ مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤُكَ أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيْتَ بِهِ نَفْسَكَ أَوْ عَلَّمْتَهُ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ أَوْ أَنْزَلْتَهُ فِي كِتَابِكَ أَوْ اسْتَأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الْغَيْبِ عِنْدَكَ أَنْ تَجْعَلَ الْقُرْآنَ رَبِيعَ قَلْبِي وَنُورَ صَدْرِي وَجِلَاءَ حُزْنِي وَذَهَابَ هَمِّي.

Allahumma inni abduka wa ibnu abdika wa ibnu amatik, naasiyati biyadika, maadhin fiyya huk`muka, adlun fiyya qadhauka, as`aluka bikulli ismin huwa lak, sammayta bihi nafsak,  au anzaltahu fi kitabik, au allamtahu ahadan min khalqiq, awista`tharta bihi fi ilmi l`ghaibi indak, an taj`aal lqur`ana rabia qalbi, wa nura sadri, wa jila`a huzni, wa dhahaba hammi.

Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu mimi ni mja Wako, mtoto wa mja Wako (mwanamume), na mtoto wa mja Wako (wa kike), utosi wangu uko mikononi Mwako, niliyoyafanya yako katika hukumu yako, uadilifu ni katika kuhukumu kwako, nakuomba kwa kila jina Lako ulilojiita Mwenyewe, au uliloliteremsha katika kitabu Chako, au ulilomfundisha yoyote yule katika viumbe Vyako, au ulilolihifadhi katika ilimu iliofichika iliyoko Kwako, nakuomba ujaaliye (uifanye) Qur’ani sababu ya kuuchipuza moyo wangu[2]. na nuru ya kifua changu, na sababu ya kuondoa huzuni yangu, na kuondoa majonzi yangu”. Halafu akaendelea akasema, “

إِلَّا أَذْهَبَ اللَّهُ هَمَّهُ وَحُزْنَهُ وَأَبْدَلَهُ مَكَانَهُ فَرَجًا قَالَ فَقِيلَ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَلَا نَتَعَلَّمُهَا فَقَالَ بَلَى يَنْبَغِي لِمَنْ سَمِعَهَا أَنْ يَتَعَلَّمَهَا.

Maana yake, "Isipokuwa Mola Mtukufu atamuondolea masikitiko na huzuni yake na Atambadilishia badala yake faraja. Akasema, "Ikasemwa Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu jee tujifundishe? Akasema, "Ndio inahitaji kila atakaesikia ajifundishe". 

Na ikiwa anaeomba ni mwanamke basi aseme, "

اللَّهُمَّ إِنِّي أمتك وَابْنُة عَبْدِكَ وَابْنُة أَمَتِكَ نَاصِيَتِي بِيَدِكَ مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤُكَ أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيْتَ بِهِ نَفْسَكَ أَوْ عَلَّمْتَهُ أَحَدًا مِنْ خَلْقِكَ أَوْ أَنْزَلْتَهُ فِي كِتَابِكَ أَوْ اسْتَأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الْغَيْبِ عِنْدَكَ أَنْ تَجْعَلَ الْقُرْآنَ رَبِيعَ قَلْبِي وَنُورَ صَدْرِي وَجِلَاءَ حُزْنِي وَذَهَابَ هَمِّي.

Allahumma inni amatika wa ib`nata abdika wa ib`nata amatika, naasiyati biyadika, maadhin fiyya huk`muka, adlun fiyya qadhauka, as`aluka bikulli ismin huwa lak, sammayta bihi nafsak,  au anzaltahu fi kitabik, au allamtahu ahadan min khalqiq, awista`tharta bihi fi ilmi l`ghaibi indak, an taj`aal lqur`ana rabia qalbi, wa nura sadri, wa jila`a huzni, wa dhahaba hammi.

Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu mimi ni mja Wako mwanamke, na mtoto wa mja Wako (mwanamume), na mtoto wa mja Wako (wa kike), utosi wangu uko mikononi Mwako, niliyoyafanya yako katika hukumu yako, uadilifu ni katika kuhukumu kwako, nakuomba kwa kila jina Lako ulilojiita Mwenyewe, au uliloliteremsha katika kitabu Chako, au ulilomfundisha yoyote yule katika viumbe Vyako, au ulilolihifadhi katika ilimu iliofichika iliyoko Kwako, nakuomba ujaaliye (uifanye) Qur’ani sababu ya kuuchipuza moyo wangu[3]. na nuru ya kifua changu, na sababu ya kuondoa huzuni yangu, na kuondoa majonzi yangu”.

 

II. Kutoka kwa Anas bin Malik R.A.A, kasema, "Mara nyingi nilikuwa namsikia Mtume S.A.W. akiomba kwa kutumia maneno haya, [4]"

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْهَمِّ وَالْحَزَنِ وَالْعَجْزِ وَالْكَسَلِ وَالْبُخْلِ وَضَلَعِ الدَّيْنِ وَغَلَبَةِ الرِّجَالِ.

Allahumma inni audhubika mina l`hammi wal`hazani, wal`ajzi, wal`kasali, wal`bukhli, wadhalai ddaini wa ghalabatir rijaal.

Maana yake, "Ewe Mola (wangu) mimi najilinda Kwako kutokana na kupata machungu ya nafsi, na huzuni, na kutokuwa na uwezo, na uvivu, na ubakhili, na uzito wa deni, na kushindwa na watu”

 

III. Kasema Ibn Abbas R.A.A., "Mtume S.A.W. alikuwa akipatwa na huzuni, akiomba (kwa kusema),[5]"

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ الْحَلِيمُ الْحَكِيمُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ رَبُّ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضِ وَرَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمُ.

Laa ilaha illa Llah, l`Haliimu L`Hakiim, laa ilaha illa Llah Rabbul`arshi l`Adhiim, laa ilaha illa Llah Rabbu ssamawaati wal`ardhi, wa Rabbu l`Arshi L`Kariim.

Maana yake, “Hapana mungu anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, Mpole mwenye Hekima, Hapana mungu anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, Mwenye kiti kikuu cha enzi[6], Hapana mungu anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah Mola wa mbingu na ardhi, na Mola wa arshi karimu" .

 

IV Kutoka kwa Ali bin Abii Talib R.A.A. kasema, "Alinilakinia[7] Mtume S.A.W. maneno yafuatayo na akaniamrisha ikiwa itanipata huzuni katika moyo wangu au shida (machungu) niyaseme [8], "

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ الْكَرِيمُ الْحَلِيمُ سُبْحَانَهُ وَتَبَارَكَ اللَّهُ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ.

La ilaha illa Llah, l`Kariimu L`Haliimu sub`hanahu wa tabaaraka Llahu Rabbu L`Arshi L`Adhiim, wal`hamdulillahi Rabbi l`alamiin.

Maana yake, "Hapana mungu anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, Mkarimu, Mpole ametakasika ametukuka Mwenyezi Mungu, Mwenye kiti kikuu cha enzi[9], na sifa njema na shukrani zote ni Zake Mola Mlezi wa viumbe vyote (Walimwengu)".

 

V. Kasema Bibi Asmaa bint Umeish R.A.A.H., "Kasema Mtume S.A.W.,[10] "Nikufundishe maneno uyaseme wakati wa huzuni au katika masikitiko, "

أَللَّهُ أَللَّهُ رَبِّي لَا أُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا.

Allahu Allahu Rabbi la ushriku bih shai`an.

Maana yake, "Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Mola wangu simshirikishi na chochote"

 

Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Suratul Anbiyaa aya ya 87 na aya ya 88, "

Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika, na akadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza, "

﴿لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنَ الظَّالِمِينَ﴾.

Laa ilaha illa Anta Subhaanaka Innii kuntu mina dh-dhalimiin.

Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo tunavyo waokoa Waumini".

 [1] Ahmad 8/63 (3528).

[2] Kuupa utulivu, na furaha.

[3] Kuupa utulivu, na furaha.

[4] Ttrmidhy 11/388 (3406).

[5] Ttirmidhiy 11/322 (3357).

[6] Inakusudiwa Yeye Allah ndiye Mmiliki na Muumba wa kila kitu. Tafsiri ya Ibn Kathir Kiswahili ya Surat Ttawba.

[7] Kunisemezesha, Kunifundisha.

[8] Ahmad 2/194 (688).

[9] Inakusudiwa Yeye Allah ndiye Mmiliki na Muumba wa kila kitu. Tafsiri ya Ibn Kathir Kiswahili ya Surat Ttawba.

[10] Abu Dawud 4/321 (1304)

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment