Ibadhi.com

12. DUA AKIWA NDANI MSIKITINI.

I. Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat AN-Nur aya ya 36, "

﴿فِي بُيُوتٍ أَذِنَ اللَّهُ أَن تُرْفَعَ وَيُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ يُسَبِّحُ لَهُ فِيهَا بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ.

Maana yake, "Katika Nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe, na humo litajwe jina Lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni".

 

II. Kasema Anas bin Malik R.A.A., "Kasema Mtume S.A.W. kumwambia bedui mmoja aliekojolea msikitini, [1]"

﴿إِنَّ هَذِهِ الْمَسَاجِدَ لاَ تَصْلُحُ لِشَىْءٍ مِنْ هَذَا الْبَوْلِ وَلاَ الْقَذَرِ ، إِنَّمَا هِىَ لِذِكْرِ اللَّهِ تَعَالَى وَالصَّلاَةِ ، وَقِرَاءَةِ الْقُرْآنِ.

Maana yake, "Hakika msikiti huu haifalii chochote[2] kwa mkojo huu na wala uchafu, hakika wenyewe (yaani msikiti) ni kwa ajili ya kumdhukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa ajili ya Sala, na kusoma Quraani".

 

III. Kutoka kwa Abu Huraira R.A.A. kasema, "Kasema Mtume S.A.W.,[3] "

مَنْ سَمِعَ رَجُلًا يَنْشُدُ ضَالَّةً فِي الْمَسْجِدِ فَلْيَقُلْ لَا رَدَّ اللَّهُ عَلَيْكَ فَإِنَّ الْمَسَاجِدَ لَمْ تُبْنَ لِهَذَا.

Maana yake, "Atakae msikia mtu anaulizia kitu chake kilichopotea msikitini, basi amwambie, "Allah asikurejeshee, kwani misikiti haikujengwa kwa ajili hii (kutangazia au kutafutia kilichopotea)."

 

IV. Kutoka kwa Ibn Abbas R.A.A. kasema, "Kasema Mtume S.A.W. ,[4]

طُهِّرَتِ الْمَسَاجِدُ مِنْ ثَلاَثٍ: مِنْ أَنْ يُنْشَدَ فِيهَا بِالضَّوَالِّ ، أَوْ يُتَّخَذَ فِيهَا طَرِيقٌ، أَوْ يَكُونَ فِيهَا سُوقٌ.

 Maana yake, “Imetoharishwa misikiti na mambo matatu: kutangazia vitu vilivyopotea, kuifanya ni barabara (kwa mfano unakwenda mahala unaingia msikitini na kufanya ndio njia) au kufanya soko la kufanyia biashara.”

 

V.  Kwa ule utukufu wa misikiti inatakiwa kila Muisilamu aitukuze na kuipa heshima yake inayostahiki, na akifanya hivyo ni kheri na bora kwake, na ni dalili ya kuonyesha ucha-Mungu wake. Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Haji aya ya 30, "

﴿وَمَنْ يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَهُ عِنْدَ رَبِّهِ.

Maana yake, "Na anaye vitukuza vitakatifu vya Mwenyezi Mungu basi hayo ndiyo kheri yake mbele ya Mola wake Mlezi".

 

VI. Pia Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Haji aya ya 32, "

﴿وَمَنْ يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِنْ تَقْوَى الْقُلُوبِ.

Maana yake, "Na anayetukuza alama za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo".

Hivyo basi inavyotakiwa kila aingiae msikitini asifanye humo kila kilichokatazwa, kama vile kutangaza biashara, au kitu kilichopotea, na kadhalika. Badala yake akiwa humo ajishughulishe na yale yanayomridhia Allah katika ibada, kusoma Quraani, na kuvuta nyiradi na kadhalika. 

 [1] Al Baihaqy (K) 2/412 (4311), Muslim 2/133 (429).

[2] Siyo mahali pake pa kujisaidia haja ndogo au kutupia uchafu.

[3] Ibn Maajah 2/482 (759).

[4] Al Rabi`u 1/82 (260).

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment