Ibadhi.com

Nini kauli yenu kwa asiyehudhuria sala ya Ijumaa, na anatoa udhuru wa umbali wa msikiti wa Ijumaa kutoka eneo analoishi, na kuwapo tafauti za kikabila baina yao na watu eneo lenye msikiti huo wa Ijumaa?

Nini kauli yenu kwa asiyehudhuria sala ya Ijumaa, na anatoa udhuru wa umbali wa msikiti wa Ijumaa kutoka eneo analoishi, na kuwapo tafauti za kikabila baina yao na watu eneo lenye msikiti huo wa Ijumaa?

Ni wajibu kwenda kwenye sala ya Ijumaa inaponadiwa katika ardhi yoyote ambayo kuiendea hukumpelekei mtu kupunguza sala kwa safari. Jabir –Allah amrehemu- alipoulizwa kukhusu sala ya Ijumaa je inamlazimu yule ambaye haisikii adhana yake? alijibu: "Lau kama hakuiendea isipokuwa mwenye kuisikia adhana yake basi wachache wangalikuwa wanaoiendea, bali iendewe kutoka masafa ya farsakhi mbili na tatu". Na Suhar bin Abbas Al Abdi –Allah amridhie- alikuwa akitoka kwenda kwenye sala ya Ijumaa tangu alfajiri na akirejea kwake wakati wa magharibi. Inakuwaje watu hawa wanatoa udhuru wa kutokwenda kwenye sala ya Ijumaa; tafauti za kikabila hazihusiani kabisa na mambo ya ibada, kwasababu ibada zimewekwa na Sharia ili ziwakusanye watu na kuwaunganisha na kuwajengea umoja. Kwa hali yoyote hawa ikiwa hawendi kwenye sala ya Ijumaa ikinadiwa watakuwa wameitupa fardhi na wamepuuza wajibu. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment