Ibadhi.com

Nini rai yenu kwa mwenye kusema: sala ya Ijumaa haisihi katika dola inayoongozwa na serikali isiyo ya kiislamu kama Tanzania?

Nini rai yenu kwa mwenye kusema: sala ya Ijumaa haisihi katika dola inayoongozwa na serikali isiyo ya kiislamu kama Tanzania?

Inatosha katika sharia ya sala ya Ijumaa kuwa kiongozi wa dola ni mtu mwenye kuamini shahada mbili za Uislamu – hata kama hatekelezi zinavoamuru. Hamuhitaji dalili zaidi ya kwamba Watangulizi wema waliisali chini ya dola ya Bani Umayya wakati hawa ndio waliobadili hukumu za Allah, na wakawakutisha waja wake wema dhulma na udhalilifu. Yawezekana pia kuitwa imamu aliye kafiri nje ya Uislamu, kwani Allah Taala kasema kukhusu Firauni na watu wake:{Na tuliwafanya maimamu (viongozi) waitao kwenye Moto}. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment