Ibadhi.com

Nini kauli yenu kukhusu kujuzu kusali sala ya Ijumaa katika msikiti wa jeshi la mipaka ya kaskazini, na kulifanya eneo hilo watan kwa wanajeshi wanaofanya kazi katika jeshi hilo, nalo ni eneo la kiaskari inazuiwa kuliingia ila kwa ruhusa kutoka kwa k

Nini kauli yenu kukhusu kujuzu kusali sala ya Ijumaa katika msikiti wa jeshi la mipaka ya kaskazini, na kulifanya eneo hilo watan kwa wanajeshi wanaofanya kazi katika jeshi hilo, nalo ni eneo la kiaskari inazuiwa kuliingia ila kwa ruhusa kutoka kwa kamanda mkuu au ofisa wa operesheni, tukijua kuwa kama itasaliwa fardhi ya Ijumaa basi watakaoisali ni wanajeshi tu na wao wote ni wasafiri?

Hamjuzii mtu kufanya watan isipokuwa pale anapoishi kwa kudumu bila wasiwasi. Imamu A'Saalimi –Allah amrehemu- kasema:Watani ya mtu ni pale anapoishi Nafsi yake ikatua akawa aishiAona pabora halimtoi ahame Ila jambo kubwa la kumkera ahameSifa hizi hazikubaliani na jeshi ulilotaja, kwani kufanya watan eneo hilo kwa wasiokuwa wakaazi wake hakujuzu. Dalili ya hayo ni matendo ya Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- na sahaba zake –radhi za Allah ziwashukie- kwani hawakuwa wakitimiza sala ila pahala wanapoishi kwa kudumu na nafsi zao zikatulia. Na wanao wajibikiwa na Ijumaa ni wakaazi, na kwa sala hiyo sala ya adhuhuri huondoka kwa makubaliano ya wote. Ama wakiwa wote ni wasafiri basi wao hawakupangiwa kisharia waisali, kwa dalili ya kwamba Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- hakuisali katika safari zake, na ilikuwa imemsudufia Ijumaa siku ya Arafa katika hija ya maagano na walikuwa pamoja naye idadi kubwa ya Waislamu, akasali adhuhuri na wakasali pamoja naye vivyo hivyo. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment