Ibadhi.com

Nini kauli yenu kukhusu mwenye kuleta chombo cha kurikodia kanda ('tape-recorder') siku ya Ijumaa msikitini na akatia kanda ya Qur'ani ambamo watu wanasema nyuma msomaji ibara ya kupendezewa "Allah Allah ya sheikh!", je hili linajuzu?

Hali hii ni katika bidaa ambazo watu wanatakiwa waziwache, kutokana na kuwa zinasababisha ubabaishaji wa wanaotaka kusali sala ya maamkizi ya msikiti, na wanaotaka kumdhukuru Allah kati ya waliohudhuria, bali aula kila mmoja asome Qur'ani peke yake. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment