Ibadhi.com

Mstahiwa Sheikh: kama mtu amekuja kusali Ijumaa, na wakati anasikiliza khutba akakumbuka kuwa ana janaba akasema katika nafsi yake ntasikiliza khutba kisha baada ya kumaliza ntaoga na kurudia sala, lakini alisahau kuirudia

Mstahiwa Sheikh: kama mtu amekuja kusali Ijumaa, na wakati anasikiliza khutba akakumbuka kuwa ana janaba akasema katika nafsi yake ntasikiliza khutba kisha baada ya kumaliza ntaoga na kurudia sala, lakini alisahau kuirudia na alikumbuka baada ya siku tatu, nini kinamlazimu? Tupe fatwa nawe upate ujira.

Mwenye kukumbuka kuwa ana janaba naye yumo msikitini kwa ajili ya sala ya Ijumaa au nyengineyo inamlazimu atoke papo hapo akaoge, kwasababu janaba inazuia kisharia mtu kuingia msikitini au kubaki humo. Kubaki kwake humo kwa ajili ya kusikiliza khutba kunakuwa ni kosa kwa pande mbili: kwanza ni kuuvunjia heshima msikiti kwa kubaki kwake humo hali ya kuwa ni mwenye janaba, na pili ni kwa kujikosesha sala ya Ijumaa ambayo imemwajibikia, kwasababu haisihi katika hali ya kuwa na hadathi, naye ana hadathi kubwa katika hali hii. Kwa hiyo inamlazimu kulipa sala yake na kutubu kwa Allah kutokana na alivofanya. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment