Ibadhi.com

Ninapokwenda kusali sala ya Ijumaa nahisi dhiki sana wakati wa kukaa kusikiliza khutba, kwasababu ya maradhi yaliyo mwilini mwangu, na siwezi kukaa mkao kama wa tashahudi, kwa ajili hiyo nahitaji kubadilisha mkao zaidi ya mara moja, je linanijuzia hi

Ninapokwenda kusali sala ya Ijumaa nahisi dhiki sana wakati wa kukaa kusikiliza khutba, kwasababu ya maradhi yaliyo mwilini mwangu, na siwezi kukaa mkao kama wa tashahudi, kwa ajili hiyo nahitaji kubadilisha mkao zaidi ya mara moja, je linanijuzia hilo, au linahisabika hilo katika yasiyo maana ? Na je katazo la kusema wakati wa khutba ni la kuharamisha au kutakasa ? Na je katika maneno yaliyokatazwa kunaingia kumtaja Allah, au ni maneno yanayozungumzwa baina ya mtu na mwengine ?

Haikatazwi kukaa mkao tafauti na anavyokaa mwenye kusoma tashahudi, na kwa kuwa kusudio la khutba ni kuwaidhi waliohudhuria basi kusema kunakatazwa wakati wa khutba –ikiwa anakosa kuisikiliza khutba- na katazo hili ni la kuharamisha, na kwa ajili hiyo imekuja katika hadithi « atakayemwambia ndugu yake wakati imamu anakhutubu 'sah’ –yaani nyamaza- basi huyo amesema upuuzi, na mwenye kusema upuuzi hana Ijumaa », na kumtaja Allah inapasa kuwe kwa moyo wakati wa khutba siyo kwa ulimi. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment