Ibadhi.com

Je inasihi kwa imamu kuwaamuru maamuma katika sala ya Ijumaa baada ya kumaliza khutba waweke sawa safu zao na washikamane?

Je inasihi kwa imamu kuwaamuru maamuma katika sala ya Ijumaa baada ya kumaliza khutba waweke sawa safu zao na washikamane?

Imamu kuwaamuru maamuma waweke sawa safu zao ni katika sunna, kwa kuwa hilo limethibiti kutoka kwa Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- iwe katika Ijumaa au sala nyengine. Vile vile maamuma anaweza kumuamuru wengine kati ya maamuma kuweka sawa safu zao, kwasababu hilo ni katika kusaidiana katika kheri. Imekuja kutoka kwa Ibnu Mahboub –Allah amrehemu- kuwa maamuma anaweza kusema baina ya iqama na sala siku ya Ijumaa 'sogea mbele wewe fulani' au 'rudi nyuma wewe' akiona pengo katika safu, na kwamba hilo haliathiri katika sala yake. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment