Ibadhi.com

Sisi ni jamaa tunasali sala ya Ijumaa katika msikiti wa Ma'bela na idadi yetu ni watu thalathini. Je tusali humo sala ya Ijumaa au twende Seeb kwenye msikiti wa karibu unaosaliwa Ijumaa, au tusali siku ya Ijumaa sala ya adhuhuri?

Inakuwajibikieni muiendee Ijumaa inakosimamishwa, na haikujuzieni kusali adhuhuri madamu Ijumaa inasimamishwa, bali inakuuwajibikieni kuiendea hata mpaka farsakhi mbili au zaidi kama alivyosema Jabir Allah amrehemu: "Iendewe kutoka farsakhi mbili na tatu". Na msichelewe kufanya hivyo wala msijitenge mkaisimamisha Ijumaa peke yenu, kwani Ijumaa si kama sala nyenginezo maana haisaliwi zaidi ya pamoja ila kwa dharura isiyokuwa na budi, kwasababu imeletwa na Sharia ili ijumuishe watu, na kuisali zaidi ya pamoja kunapingana na kujumuisha. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment