Ibadhi.com

Mstahiwa Sheikh, je inajuzu msafiri awasalishe wakaazi sala ya Ijumaa? Na je kuna ubaya iwapo imamu atamwambia muadhini baada ya khutba aqimi'ssalaah?

Mstahiwa Sheikh, je inajuzu msafiri awasalishe wakaazi sala ya Ijumaa? Na je kuna ubaya iwapo imamu atamwambia muadhini baada ya khutba aqimi'ssalaah? Na akiwapo aliye fasihi kuliko imamu je anaweza kukhutubu badala ya imamu? Na nini hukumu ya kutaja mpokezi wa hadithi mwisho wa kutaja hadithi katika khutba ya Ijumaa?

Kuna khilafu kukhusu msafiri kusalisha Ijumaa, kundi fulani katika maulama wanaona haifai, na hiyo ndiyo rai ya Imamu Nurdin A'Saalimi –Allah amridhie- katika Alhujaj Almuqni'a kwa kuwa msafiri haimlazimu sala ya Ijumaa, na kuna kauli kuwa inajuzu nayo ndiyo rai ya maulama wawili wakubwa: Hashim na Musa –Allah awarehemu- na ameisahihisha Mhakiki Al Khalili –Allah amridhie- nayo ndiyo sahihi zaidi kwangu, kwasababu msafiri ingawa haimlazimu Ijumaa lakini anawajibika kusali - sawa ikiwa ataitekeleza sala hiyo kama ni adhuhuri au Ijumaa, na sala ya Ijumaa ikiwadia na kukimiwa inakuwa wajibu juu yake, kwa hali hii kusalisha kwa msafiri kunatafautika na kusalisha mwenye kusali sunna wanosali fardhi.Ama mwenye kukhutubu kumwamrisha muadhini akimu sala baada ya kumaliza khutba halikatazwi.Na kukhutubu mtu na kusalisha mwengine bila udhuru, hili ni katika ambayo yamekuwa na khilafu, na rai inayofuatwa kwetu ni kujuzu.Na kutaja waliopokea hadithi kwa Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- katika khutba haikatazwi, lakini bora kuto kutaja sanad kwa ajili ya kufupisha kama hadhithi ni shahihi, na kutaja sanad hakuathiri kitu katika khutba. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment