Ibadhi.com

Nini kauli yenu Mstahiwa Sheikh kukhusu mtu anayewasalisha watu sala ya Ijumaa na hali wao wanamchukia ; wanachukia kusikiliza hutuba yake kwa kuwa ina mafumbo na kero kwa hisia za Waislamu,

Nini kauli yenu Mstahiwa Sheikh kukhusu mtu anayewasalisha watu sala ya Ijumaa na hali wao wanamchukia ; wanachukia kusikiliza hutuba yake kwa kuwa ina mafumbo na kero kwa hisia za Waislamu, na wanachukia kusali nyuma yake kwasababu ya mwendo wake usioridhisha. Je inawajuzia hao wanaosali waende mji mwengine inakosaliwa Ijumaa au inawalazimu wasali nyuma yake nao hawaridhiki naye wala na sala yake ?

Sala ya Ijumaa inapasa iwe yenye kujumuisha siyo yenye kufarikisha, na yenye kuunganisha siyo yenye kukimbiza, kwani Sharia imepanga kuwe na mkusanyiko katika Ijumaa na mengineyo kwa ajili kuunganisha nyoyo, kuondoa bughudha, kumaliza sababu za kutafautiana na kun’goa mizizi ya chuki. Kuitumilia hutuba ya Ijumaa kwa ajili ya kukimbiza watu na kupandikiza chuki na uadui ni jambo ambalo Uislamu hauliridhii wala haulikubali. Na yule ambaye hii ndiyo tabia yake anastahili iwe kusali nyuma yake kunachukiwa kutokana na kuchukiwa uimamu wake. Imekuja katika hadithi kutoka kwa Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- « Watatu Allah amewalaani : mtu anayewasalisha watu na hali wao wanamchukia, na mwanamke anayepitiwa na usiku na hali mumewe amekasirika naye, na mwanamme aliyesikia hayya ala’salaati hayya ala’lfalaahi kisha hakuitika ». Na kwa hiyo mimi naona uombwe upande unaohusika kumzuia mwenye kuitumilia hutuba ya Ijumaa utumiliaji huu mbaya, na awekwe badala yake yule ambaye anajulikana kwa kuwa na hadhari katika anayoyasema katika hutuba. Na Allah Ndiye Mwenye kufanikisha.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment