Ibadhi.com

Je inasihi kwa imamu aliyepangiwa msikiti awache kuwasalisha watu adhuhuri siku ya Ijumaa kwa ajili ya kwenda kunakosaliwa sala ya Ijumaa

Je inasihi kwa imamu aliyepangiwa msikiti awache kuwasalisha watu adhuhuri siku ya Ijumaa kwa ajili ya kwenda kunakosaliwa sala ya Ijumaa ?

Akiwa katika pahala panaposaliwa Ijumaa haisihi kwake kubaki katika msikiti huo awasalishe watu adhuhuri, kwani hakuna adhuhuri siku ya Ijumaa katika mji unaosaliwa Ijumaa, isipokuwa tu pakiwa pana udhuru unaozuia kwenda kusali Ijumaa, basi mwenye udhuru anaruhusiwa kusali adhuhuri. Katika yaliyonukuliwa kwa Abu Sufyan Mahboub bin A'Ruhail –Allah amrehemu- kasema: Watu wa Oman walimwandikia Jabir bin Zaid –Allah amrehemu- wakimuomba fatwa kukhusu Ijumaa, je inamlazimu aiendee yule ambaye haisikii adhana yake? Akawajibu: Kama hawaiendei ila wanaosikia adhana yake wangalikuwa wachache wanaoiendea; bali inaendewa kutoka masafa ya farsakhi mbili na tatu. Na imejulikana kwa waliotangulia –Allah awarehemu- hima yao iliyofikia kikomo ya kuhudhuria Ijumaa. Sohar bin Al Abbaas Al Abdi –Allah amrehemu- alikuwa akitoka kwenda kunako sala Ijumaa tangu baada ya sala ya alfajiri, na baada ya kumaliza sala ya Ijumaa anafunga safari kurudi nyumbani kwake, na hafiki kwake ila baada ya sala ya magharibi. Karibu na hayo yanasimuliwa pia kwa Jabir, Abu Ubaida na Haajib –Allah awarehemu. Kwa hiyo hakuna maana ya kupuuza kwa wanaopuuza kusali Ijumaa, kwani kuna kamio kali juu ya hilo katika hadithi kadha sahihi. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment