Ibadhi.com

Je khutba ya Ijumaa ni khutba mbili au khutba moja katika enzi ya Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie ?

Je khutba ya Ijumaa ni khutba mbili au khutba moja katika enzi ya Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie ?

Kutosheka kwa khutba moja ni kutosheka kwa kilichokuwa fardhi, na kuzidisha khutba ya pili kwa mwenye kufuata hilo ni kufuata Sunna. Imethibiti kutoka kwa Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- kuwa yeye alikuwa akikhutubu khutba mbili na akikaa baina yake. Na ilikuwa ikifuatwa hivyo kwa Maimamu wa Kirustum –Allah awarehemu- kama ilivo katika kitabu cha Jawaahir cha Albarraadi, na ikatajwa wazi na maulama kadha, akiwamo mwenye kitabu cha Alqanaatir katika kauli yake: "Nazo ni khutba mbili baina yake kuna kikao khafifu".Imamu Abu Is'haaq Al Hadhrami kasema katika Mukhtasar Al Khisaal: "Mnamokhutubiwa khutba mbili ni mambo mane: la kwanza ni Ijumaa …". Na Imamu A'Saalimi –Allah amrehemu- kasema katika Madaarij Al Kamaal:Kwa Ijumaa, arafa, na idi mbili Kunahutubiwa humo hutuba mbiliChapendeza kinyamazo baina yake Ili kiwe ndiyo kitenganishi chakeAl'al-laama Abu Al Hasan Al Bisyawi amesimulia katika juzuu ya pili ya Jaami' yake kwamba ijmai imepita juu ya kuwekwa sharia ya khutba mbili na kukaa baina yake, na akanukuu maneno yake kama yalivyo Al'al-laama Abu Muslim katika Nithaar Aljawhar. Vile vile ametaja khutba mbili Imamu A'Thamiini katika A'Niili, na Sheikh Aamur katika Al-iidhaah, na Sheikh Ismaaiil katika Qawaaid, na wengi wengineo. Nami nimelitafiti suala hili utafiti mpana katika risala niliyoiandika makhsusi kwa ajili yake, na nikaondoa utatanishi ulioganda katika akili za baadhi ya watu kukhusiana na suala hili. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment