Ibadhi.com

Je inajuzu sala ya Ijumaa kwa watu kumi na mbili ?

Je inajuzu sala ya Ijumaa kwa watu kumi na mbili ?

Sala ya Ijumaa ina masharti, kati yake:Mji; kwani inatakiwa isimamishwe katika mji mkubwa na isisimamishwe katika vijiji vidogo.Idhini ya mtawala.Kuwapo jamaa watakaoisimamisha. Kumekuwa na khilafu kukhusu idadi ya watu inayosihi kusali Ijumaa, ikasemwa inasihi kwa watu wawili, na kuna kauli kwa watatu, na kauli kwa kumi na mbili, na kauli kwa kumi na tatu, na kuna kauli kwa arubaini nayo ndiyo aghlabu ya rai, na kuna kauli kwa khamsini. Lakini kauli hizi hazina dalili zinazoweza kutegemewa. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment