Ibadhi.com

Ili kukamilisha faida, tunanukuu fatwa ya Mstahiwa Sheikh juu ya suali jengine linalofanana ambamo anasema:Maulama ingawa wamekhitalifiana katika shuruti zake

Ili kukamilisha faida, tunanukuu fatwa ya Mstahiwa Sheikh juu ya suali jengine linalofanana ambamo anasema:Maulama ingawa wamekhitalifiana katika shuruti zake – yaani shuruti za sala ya Ijumaa – hawakukhitalifiana katika asili ya kuwajibika kwake. Na kwa hiyo sala ya Ijumaa imethibiti kwa Kitabu cha Allah na Sunna na Ijmai. Khilafu iliyokuja katika shuruti zake inaondoshwa na amri ya Mtawala Muislamu ya kusimamishwa Ijumaa. Hivyo, ikisimamishwa kwa amri ya Mtawala haijuzu kwa ye yote kuwacha kuihudhuria, na inapasa wanaowacha kuhudhuria wapewe adabu, kwani Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- aliazimia kuzichoma moto nyumba za wasiohudhuria sala ya Ijumaa. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment