Ibadhi.com

Je inamlazimu Muislamu kusali 'tahiyyat al masjid’ (rakaa mbili za maamkizi ya msikiti) akiingia wakati imamu anakhutubu siku ya Ijumaa ?

Je inamlazimu Muislamu kusali 'tahiyyat al masjid’ (rakaa mbili za maamkizi ya msikiti) akiingia wakati imamu anakhutubu siku ya Ijumaa ? Na kama imamu anayekhutubu siku ya Ijumaa amechelewa kidogo je atakuwa na kosa akikiuka shingo za waliokuja kusali ili afike kwenye membari kwa kutokuwapo mlango unaomfikisha kwenye membari bila kukiuka shingo za watu ?

Maulama wamekhitalifiana kukhusu kusali ('tahiyyat al masjid’) mwenye kuingia msikitini wakati imamu anakhutubu, na kauli yenye nguvu inajuzu kusali bali inapendelewa, kutokana na hadithi ya Sulaik Al Ghatafaaniy kwa Masheikh Wawili (Al Bukhari na Muslim), na hakuna ubaya katika kukiuka shingo za watu kwa imamu anayekhutubu siku ya Ijumaa akichelewa kuja msikitini. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment