Ibadhi.com

Kwa vile amri ya kusimamishwa Ijumaa imekuja katika Qur’ani kwa ujumla, na haikufungamanishwa na pahala maalumu wala haikushurutishwa kwa hali maalumu, na vivyo hivyo Sunna, ni sifa gani makhususi uliyopewa mji wa Juwatha hata ukawa pahala pa pili ba

Kwa vile amri ya kusimamishwa Ijumaa imekuja katika Qur’ani kwa ujumla, na haikufungamanishwa na pahala maalumu wala haikushurutishwa kwa hali maalumu, na vivyo hivyo Sunna, ni sifa gani makhususi uliyopewa mji wa Juwatha hata ukawa pahala pa pili baada ya Madina kusimamishwa Ijumaa katika enzi yake –rehma za Allah na amani zimshukie- na haikusimamishwa katika mji wa Makka ambao umekuwa baada ya Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- miongoni mwa miji saba iliyochaguliwa kwa Ijumaa kwa makubaliano ya wote ?

Kusimamishwa Ijumaa katika Juwatha pasina Makka katika enzi ya Mtume wa Allah –rehma za Allah na amani zimshukie- ingawa Makka ilichaguliwa baadae katika miji ya Ijumaa kwa makubaliano ya wote, kunatokana na kuangalia mazingira na hali zilivyokuwa, na kwa hiyo inabainika kuwa jambo la Ijumaa katika kupanga mwahala mwa kuisimamisha linatokana na jitihada ya mawazo kwa mujibu wa inavopasa kimazingira na inavohitaji kifikra. Na Allah Ndiye Mtoaji mafanikio.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment