Ibadhi.com

Je inajuzu kusimamishwa sala ya Ijumaa katika misikiti kadha katika mji mmoja ? Kwani watu walikuwa wakisimamisha Ijumaa katika msikiti mmoja, kisha ukajengwa mwengine wakataka baadhi yao kusimamisha Ijumaa katika msikiti wa pili, je wanaruhusiwa na

Je inajuzu kusimamishwa sala ya Ijumaa katika misikiti kadha katika mji mmoja ? Kwani watu walikuwa wakisimamisha Ijumaa katika msikiti mmoja, kisha ukajengwa mwengine wakataka baadhi yao kusimamisha Ijumaa katika msikiti wa pili, je wanaruhusiwa na Sharia kufanya hivo ?

Kama msikiti wa mwanzo unatosha kwa wote wanaosali hakuna maana ya kusimisha Ijumaa ya pili, kwasababu kusudio la Ijumaa ni kujumuika, na kutawanyika kunapingana na lengo hili. Kisha inajulikana kuwa watu katika enzi ya Mtume wa Allah –rehma za Allah na amani zimshukie- walikuwa wakiiendea Ijumaa inayosimamishwa katika msikiti wake mtukufu, na ingekuwa Ijumaa kama sala nyenginezo angewaamuru waisimamishe katika mwahala mwao kama wanavyotekeleza fardhi nyenginezo. Waliporuhusu maulama kusimamishwa Ijumaa zaidi ya moja ni katika hali isiyo budi tu siyo nyengine. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment