Ibadhi.com

Nimetazama katika vitabu vya waliotangulia na waliofuatia tangu kuja kwa Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- mpaka zama za maulama waliokuja mwishoni, nikawakuta wanakataza kusaliwa sala ya Ijumaa katika Oman isipokuwa huko Sohar na Nizwa

Nimetazama katika vitabu vya waliotangulia na waliofuatia tangu kuja kwa Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- mpaka zama za maulama waliokuja mwishoni, nikawakuta wanakataza kusaliwa sala ya Ijumaa katika Oman isipokuwa huko Sohar na Nizwa. Huo ndio mwendo wa watangulizi wetu na maulama wetu ambao tunafuata nyayo zao na ruwaza yao, na sijui nini kilichobadilisha jambo hili. Je kuna sharia mpya au watu wanafanya makosa ? Niongoze unipe fatwa, Nami najikinga kwa Allah na nia ya kujionesha. 

Kutoka wapi umayapata madai haya ? Na lini umeona kuwa sala ya Ijumaa tangu enzi ya Mtume wa Allah –rehma za Allah na amani zimshukie- haisimamishwi ila katika mji wa Sohar na Nizwa ? Na kwa kitabu gani na sunna gani Ijumaa imefungamanishwa na mwahali muwili humo pasina pengine. Allah Taala anasema : {Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Allah} na hakuifungamanisha amri hiyo na Sohar wala Nizwa. Na Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- anasema : « Lazima watu waache kuziepuka sala za Ijumaa au Allah atazipiga muhuri nyoyo zao kisha watakuwa miongoni mwa walioghafilika ». Pia kasema : « Atakaeacha Ijumaa tatu kwa dharau Allah ataupiga chapa moyo wake ». Kisha Waislamu hawakukhitalifiana katika msingi wa kuwajibika sala ya Ijumaa, bali wamekhitalifiana katika shuruti zake, na rai zao zote zimetegemea jitihada zao siyo maandiko ya Sharia. Na Waislamu wameisali mwahala kadha katika Oman. Katika zama za Imamu Umar bin Al Khattaab Al Kharusi –Allah amrehemu- katika karne ya tisa ya hijra sala ya Ijumaa ilisimamishwa katika pande zote za Oman. Na Imamu Muhammad bin Sulaiman Al Mufarriji ametaja isimamishwe Ijumaa hata katika miji ya mbali na miji iliyo baina ya majabali, na barua yake inayokhusu hayo ipo. Katika enzi ya Imamu Muadilifu – Azzan bin Qais –Allah amrehemu- aliisali Ijumaa katika Maskati na Nizwa na Samad na Fanja na Ja’laan, na kila pahala alipofika ambamo Ijumaa ilimsudufia. Na katika zama za Imamu Muhammad bin Abdullah Al Khalili –Allah amrehemu- aliamuru isimamishwe Ijumaa katika Ja’laan, na ilikuwa katika rai yake kuwafiki isimamishwe katika pande zote za Oman, kama alivotaja hivo katika barua yake aliyoituma kwa Masheikhe wawili Majid bin Khamis Al Abri na Ibrahiim bin Said Al Abri. Ikiwa yamekuchanganyikia yaliyotajwa kukhusu hayo katika vitabu vya watu wetu ya uchaguzi wa miji uliofanywa na Umar bin Al Khattaab –Allah amridhie- kwa ajili ya Ijumaa, basi hayo yametokana na yeye kuangalia hali halisi ilivyokuwa na wala Nizwa haikuwa miongoni mwa miji aliyoichagua, na maimamu wa uadilifu waliisimamisha Ijumaa katika mji huo, na sikia kukhusu hayo alivyosema Imamu A’Saalimi –Allah amrehemu- katika kubainisha hikima ya kuchagua miji kwa sala ya Ijumaa :Ni hali ya kupita tu miji kupangwa Mara yaimarika na mara yagonjwaHii Sohari baada ya kuezika Na baada ya nguvu na kuimarikaSasa kama duni ya miji ikitajwa Na Maskadi badala yake imejengwaUchaguzi wa Faruqu wa hiyo miji Kwa kuwa zama zake ni bora ya mijiKama ni sharia hiyo kuchaguliwa Angechagua Nabii MteuliwaBasi wapi umekuta madai haya kwamba Waislamu wamezuia Ijumaa isipokuwa katika Nizwa na Sohar, hata ukafanya jambo baya mno uliposema : Je kuna sharia mpya au watu wanafanya makosa ? Je kwani wewe unaona hii ni sharia mpya, au pazia la ujinga limekuzinga usione ukweli.Kama hukuuona mwezi wakubalie Waliouona kwa macho usikatae

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment