Ibadhi.com

Ni hoja gani iliyowafanya maulama wa zama hizi watoe fatwa ya kuwajibika kusimamishwa sala ya Ijumaa katika miji yote ya Oman ?

Ni hoja gani iliyowafanya maulama wa zama hizi watoe fatwa ya kuwajibika kusimamishwa sala ya Ijumaa katika miji yote ya Oman, pamoja na kuwa katika zama za maimamu na maulama waliotangulia haikuwa ikisimamishwa ila katika miji miwili ya Nizwa na Sohar, na hawakuamuru isimamishwe katika miji mengineyo ? Na je ana kosa anayeiacha katika miji isiyokuwa miwili hii ? Tupe fatwa ya jawabu nawe upate thawabu.

Sala ya Ijumaa ni katika fardhi zilizothibiti kwa maandiko ya wazi ya Kitabu cha Allah kitukufu na Sunna ya Mtume na ijmai ya maulama wa Umma. Na hakuna katika Kitabu cha Allah wala katika Sunna ya Mtume yanayoonesha imekhusishwa na miji maalumu pasina mengine. Ikiwa hali na mazingira katika zama zilizotangulia yalifanya iamulike kusaliwa Ijumaa Nizwa na Sohar katika Oman, hayo hayabaki hivo wakati wote. Je kuna andiko lo lote au ijmai kwamba isaliwe mwahala maalumu pasina pengine ? Isitoshe sisi tunakuta kuwa waislamu hawakuisali katika mji wa Nizwa wakati wa Imamu Alwaarith bin Ka’ab –Allah amridhie- na hali waliisimamisha humo maimamu waliokuja baada yake –Allah awarehemu. Vilevile imamu muadilifu shahidi Azzan bin Qais –Allah amrehemu- aliisimamisha kila anapokwenda katika ardhi ya Oman. Kisha uchaguzi wa miji kwa sala ya Ijumaa unaotajwa kutoka kwa Alfaaruuq (Umar bin Alkhattaab) –Allah Taala amridhie- haukuwa ila tokeo la hali iliyokuwapo. Ni vizuri mno alivyosema Imamu Nurdiin A’Saalimi –Allah amridhie- kukhusu hilo, aliposema katika Jawhar yake :Ni hali ya kupita tu miji kupangwa Mara yaimarika na mara yagonjwaUchaguzi wa Faruqu wa hiyo miji Kwa kuwa zama zake ni bora ya mijiKama ni sharia hiyo kuchaguliwa Angechagua Nabii MteuliwaKwa hiyo inabainika kuwa baada ya maulama kuona isimamishwe sala ya Ijumaa katika miji mikuu ya Oman, na kuamrishwa hilo na Kiongozi wa nchi, haijuzu kuacha kuihudhuria katika mji wo wote inaposimamishwa. Na mwenye kusali adhuhuri badala yake bila udhuru hana sala. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment