Logo
Print this page

Nini dalili za kujuzu kusali sala ya Ijumaa katika miji yote ?

Nini dalili za kujuzu kusali sala ya Ijumaa katika miji yote ?

Allah ameamuru kwenda kwenye sala ya Ijumaa inaponadiwa, na hakuikhusisha kwa mahala maalumu pasina pengine wala kwa hali fulani pasina nyengine, wala haikuja sunna ya maneno yenye kubainisha cho chote kati ya hayo. Lakini Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- aliisimamisha sala hii Madina Munawara na Ijumaa ya pili ilikuwa kule Juwatha, ambako kumesemwa kuwa ni mji katika Albahrain. Kisha Umar –Allah amridhie- akaichagulia sala ya Ijumaa miji aliyoichagua, lakini haikuja kabisa dalili inayoonesha kuwa alikataza kuisali mwenginemo. Bali mwanawe –Allah amridhie- amehadithia kwamba Umar alikuwa akipita kwenye maji yaliyopo baina ya Makka na Madina na watu wa hapo wakisimamisha sala ya Ijumaa naye hawakatazi. Na Mahbuub -Allah amrehemu- amepokea kutoka kwa Suhaar au Dhumaam kuwa amesema : Kama ingalikuwa sala ya Ijumaa inasimamishwa Khuraasaan basi ingalistahiki kuendewa. Kwa ajili ya yote hayo tunaona kuwa maulama wa Waislamu wana haki ya kujitahidi katika hili, na wakiona inafaa sala ya Ijumaa kukimiwa mahala fulani na ikanadiwa itawajibika kuiendea, na haitajuzu kuacha kuhudhuria kwa kuwa imenadiwa na amri ya kuiendea katika aya ya Qur’ani imeshurutishwa kwa kunadiwa. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
All Rights Reserved.