Ibadhi.com

KURUDIA SALA NA KUILIPA : 12

Mtu amesibiwa na ugonjwa wa kupooza, na hakuweza kusali muda wa miezi mine, sasa anataka kufanya kafara kwa sala hizo ambazo hakuzisali, nini kinamwajibikia ?Sala haifanyiwi badala kwa kafara wala kinginecho, bali inamlazimu asali kwa hali yo yote hata akiwa amelala chali tandikoni pake, bali hata kama hakuweza kufanya cho chote ila kutamka takbira kwa kila sala takbira tano basi itamlazimu kufanya hivo, na hakubaliwi udhuru wa kuto kufanya hilo. Na kwa kuwa huyu hakufanya kitu kati ya hayo inamlazimu atubu kwa Allah na alipe sala zote alizozipoteza. Khilafu ipo katika kafara je inamwajibikia au la ? Na kwa kauli ya kuwajibika imesemwa kila sala ina kafara, na imesemwa ni kafara tano kwa sala zote, na imesemwa ni kafara moja, nayo ni kumpa uhuru mtumwa, asipopata uwezo basi ni kufunga miezi miwili mfululizo, asipoweza basi ni kulisha maskini sitini. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment