Ibadhi.com

KURUDIA SALA NA KUILIPA : 9

Nini kauli yenu kukhusu ambaye ameakhirisha sala mpaka wakati wa sala nyengine kwasababu ya baadhi ya makazi, je asali sala iliyopita kwanza kisha asali iliyofika, au asali iliyofika kwanza?Haimjuzii kuipitisha sala kwa ajili ya kazi yo yote, bali inamlazimu asali hata katika hali ya kukabiliana na adui katika jihadi, au hali ya kupambana kwa silaha, kama walivoeleza wanachoni wa fiqhi. Vilevile ikiwa hakuweza kujitoharisha inamlazimu asali vyovyote awezavyo, asipofanya hivo atawajibika kulipa na kutubu, na aanze kwa sala iliyopita kabla iliyofika. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment