Ibadhi.com

KURUDIA SALA NA KUILIPA : 7

Nini kauli yenu kukhusu ambaye amefanyiwa utibabu wa upasuaji, akaacha sala kwasababu ya kuto kukatika damu na kuto kuzuia mkojo, alipopona akazilipa sala alizoziacha, je kinamlazimu cho chote kwa kuacha sala katika hali ya ugonjwa?Inamlazimu kutubu kwa kuziakhirisha sala mpaka kumaliza wakati wake, kwasababu wajibu wake ulikuwa asipitishe wakati wa sala bila kusali akiwa ana fahamu zake, japokuwa jeraha lake linamiminika damu na mkojo hausiti kutoka. Kukhusu kafara kuna khilafu, na kauli sahihi zaidi ni kuto kuwajibika. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment