Ibadhi.com

KURUDIA SALA NA KUILIPA : 4

Mwanamke amesibiwa na maradhi ya kupooza, akaacha sala na saumu mpaka akafa, vipi alipiwe saumu na sala?Ilikuwa inamlazimu asali kwa mujibu wa uwezo wake hata kama kwa kulala ubavu. Kukhusu saumu ilikuwa inamlazimu alishe kwa kila siku maskini mmoja, na kwa kuwa yeye hakulisha maskini katika uhai wake basi warithi wake wamlishie. Ama sala imeshapita na haijuzu mtu kumsalia mwengine. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment