Ibadhi.com

KURUDIA SALA NA KUILIPA : 3

Nini kauli yenu kukhusu mwenye kuacha sala kwa muda kwasababu ya ugonjwa wake, kwa kuwa amefanyiwa utibabu wa upasuaji kwenye kiungo kimojawapo kati ya viungo vya udhu, ambao unamfanya ahisi maumivu makali anapotaka kusali au kutawadha, je kinamlazimu kitu?Ilikuwa inamlazimu asali kwa hali yo yote hata kama kwa kulala chali; akiwa hawezi kutawadha atatayamamu, na asipoweza yote mawili atasali bila ya yote mawili. Na kwa kuwa yeye hakusali inamlazimu kulipa sala alizoziacha pamoja na kutubu kwa Allah. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment