Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 22

Aliyejiunga na imamu katika rakaa ya pili, wakati gani atamke 'istiadha'? Na ikiwa katika suala hili kuna khilafu ipi kauli yenye nguvu kwenu?Katika hilo kuna khilafu na kauli yenye nguvu atamke 'istiadha' mara ya mwanzo anaposoma Qur'ani na imamu, kwasababu 'istiadha' imewekwa katika sharia kwa ajili ya kusoma Qur'ani; Allah Taala amesema:ﭽ ﮝ ﮞ ﮟ ﮠ ﮡ ﮢ ﮣ ﮤ ﭼ النحل: ٩٨{Na ukisoma Qur'ani mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani maluuni}Na kwa hiyo kama ataichelewesha 'istiadha' Qur'ani atayosoma na imamu itakuwa haina 'istiadha'. Kauli nyengine kwamba aicheleweshe mpaka atakapoinuka kulipa kilichomfutu, na sababu yake ni kwamba mahala pa kusoma 'istiadha' ni rakaa ya mwanzo na hiyo ndiyo rakaa ya mwanzo. Lakini kauli yenye nguvu ni ile iliyotangulia. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment