Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 21

Nimejiunga na imamu aliyenitangulia sala ya magharibi, na sikuweza kusoma alfaatiha na sura, nini kinanilazimu iwapo sikuvilipa?Katika suala hili kuna khilafu; baadhi ya maulamaa wamesema: Imamu humbebea maamuma kisomo cha Qur'ani ikiwa kimemfutu kisomo tu na hakikumfutu kinginecho. Na kuna kauli bali inamlazimu alipe kila kilichomfutu kwa imamu sawa kikiwa kilichomfutu ni kisomo peke yake au kisomo na vilivo baada yake ambavo ni rukuu na sujudu, au kisomo na rukuu tu, kwa dalili ya kauli yake –rehma za Allah na amani zimshukie- "Mlichodiriki salini na kilicho kufutuni lipeni".Na kuna katika maulamaa wanaoona kuwa imamu akimtangulia maamuma kwa kisomo basi rakaa hiyo nzima imemfutu maamuma na inamlazimu ailipe. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment