Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 20

Mwenye kumdiriki imamu katika rakaa mbili za mwisho za sala ya adhuhuri akiwa anakusudia kuchanganya baina ya adhuhuri na alasiri, je atosheke na rakaa mbili alizosali na imamu kwa sala ya adhuhuri kisha ainuke kusali rakaa mbili za alasiri au inamlazimu aitimize sala ya adhuhuri rakaa nne kwa mujibu wa sala ya imamu?Msafiri akisali nyuma ya imamu mkaazi inamwajibikia kutimiza sala ya rakaa nne, sawa akiwa amejiunga naye tangu mwanzo wa sala yake au katikati hata kama katika rakaa mbili za mwisho, kwasababu inamwajibikia amfuate imamu wake na kwa hiyo asali kama alivosali imamu. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment