Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 18

Mwenye kujiunga na sala akimdiriki imamu katika rakaa mbili za mwisho za sala ya isha, je analipa alfaatiha peke yake katika rakaa mbili zilizompita au alfaatiha na sura? Na je akiinuka kulipa anainuka kwa takbira? Na wakati gani anasoma tashahudi?Hapana budi na kusoma alfaatiha na sura katika kulipa rakaa mbili za mwanzo alizotangulia kwazo imamu katika sala ya isha, kwasababu hiyo sura pia ilimfutu aliyetanguliwa. Na anasoma tashahudi anapokaa pamoja na imamu, na akiinuka kulipa anainuka bila takbira. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment