Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 17

Kukhusu hadithi: "Aliyediriki rukuu ameidiriki sala", je inamaanisha kuzuiwa kujiunga na sala ya jamaa kwa ambaye hakudiriki rukuu?Inamjuzia kujiunga akidiriki rukuu, na khilafu ni katika yaliyo baada ya rukuu, lakini kauli yenye nguvu ni kujuzu kujiunga kutokana na ujumla wa hadithi: "Mlichodiriki salini na kilicho kufutuni lipeni", wala hakuna kikhusishi kilichoukhusisha ujumla huu na sehemu fulani ya sala pasina nyengine. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment