Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 14

Mstahiwa Sheikh, unasemaje kukhusu mwenye kuingia msikitini akakuta jamaa inasaliwa asijiunge nao bali akakaa mpaka imamu akawa katika tashahudi ya mwisho ndiyo yeye akainuka na kusali peke yake? Na muadhini akiadhini je inajuzu kwa aliyeingia msikitini kutoka kwa jambo la kidunia kabla hajasali na jamaa?Imekuja katika hadithi sahihi kutoka kwa Mtume wa Allah –rehma za Allah na amani zimshukie- "Ukija na watu wanasali sali nao". Hii inaonesha kuwa haijuzu kuacha kujiunga na jamaa ikikimiwa, kwasababu amri yake –rehma za Allah na amani zimshukie- kama amri ya Allah inamaanisha uwajibikaji isipokuwa ikitolewa katika maana hiyo na ishara fulani. Vile vile yamethibiti kutoka kwa Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- yanayoonesha ulazima wa kulipa kilichofutu katika sala kwa mwenye kujiunga na imamu wakati kimemfutu kitu katika sala, nayo ni kauli yake: "Mlichodiriki salini na kilicho kufutuni lipeni", na katika riwaya nyengine "timizeni". Haya kama yanavyoonesha ulazima wa kulipa kilichofutu yanaonesha ulazima wa kujiunga na jamaa. Kwa hiyo haisihi kwa mwenye kukuta jamaa wanasali kungoja au kutoka ili asali peke yake au na jamaa nyengine. Vile vile mwenye kuingia msikitini wakati muadhini ameshaazini haruhusiwi kutoka kabla hajasali isipokuwa kwa dharura isiyokuwa na budi, au akiwa anaweza kurudi akasali. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment