Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 12

Nini hukumu ya mwenye kuingia msikitini akakuta jamaa inasaliwa na safu ya mwanzo imekamilika, je anaweza kupita baina ya maamuma apange safu ubavuni mwa imamu, au asali peke yake nyuma ya safu, au asubiri mpaka aje mtu apange naye safu, au nini afanye?Aula amvute mmoja kati ya maamuma ili apange naye safu na wasali pamoja nyuma ya safu ya mwanzo. Na akiweza kwenda mbele mpaka akawa ubavuni mwa imamu bila ya kumuudhi ye yote kati ya maamuma hapana kosa juu yake katika hilo. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment