Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 11

Nini hukumu ya sala ya mwenye kudiriki sala kwa imamu katika tashahudi ya mwisho? Na akiondoka maamuma pahala pake baada ya imamu kutoa salamu ili akamilishe sala yake je kuna kosa juu yake?Kujiunga kwake na imamu baada ya imamu kuwamo katika tashahudi ya mwisho kuna khilafu, lakini kauli yenye nguvu kunajuzu kutokana na ujumla wa hadithi "Mlichodiriki salini". Ama kuondoka kwake pahala alipokuwa akisali baada ya imamu kutoa salamu hilo linabatilisha sala yake, na inamlazimu aianze upya baada ya kuibatilisha. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment