Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 9

Mtu akija kwa jamaa wanaosali akamkuta imamu yuko naye mtu mmoja kuliani kwake, je inamjuzia aunge safu ubavuni mwa mtu anayesimama kuliani kwa imamu, au inamlazimu amvute maamuma huyo kumleta nyuma ili wafanye safu nyuma ya imamu? Na akimvuta maamuma je halisababishi hilo kutengua sala yake (yaani sala ya mwenye kuvutwa)?Inampasa amvute maamuma kumleta nyuma na halisababishi hilo kubatilisha sala ya mwenye kuvutwa. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment