Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 8

Unasemaje Mstahiwa Sheikh kukhusu mtu aliyewahi kwa imamu rakaa mbili katika sala ya rakaa nne akasoma naye tashahudi ya mwisho mpaka "عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ" (abduhu warasuuluhu), je akilipa kilichomfutu katika sala inamlazimu kusoma tashahudi mara nyengine tangu mwanzo au kuanzia alipofika awali, au anakaa na kutoa salamu na halazimiki kusoma kitu?Akitaka kulipa kilichobaki katika tashahudi ya mwisho ambacho ni dua na kumsalia na kumsalimia Mtume wa Allah –rehma za Allah na amani zimshukie- hilo linajuzu, na akitoa salamu akikaa baada ya kulipa kilichomfutu hapana kitu juu yake. Qutbu al aimma –Allah amrehemu- amependelea mwenye kulipa kilichomfutu alete tashahudi ya mwisho kikamilifu nyuma ya imamu. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment