Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 7

Nini kauli yenu kukhusu kile anachokisali na imamu yule ambaye hakuwahi mwanzo wa sala pamoja na imamu, je hicho ni mwanzo wa sala yake na anachokileta baadae ni mwisho wa sala yake au ni kinyume cha hayo? Na je inamlazimu asome sura ikimfutu baada ya alfaatiha?Kumekuwapo khilafu kukhusu anachokisali anayejiunga na sala akiwa ametanguliwa na imamu, je hicho ni mwanzo wa sala yake na anachokileta baadae ni mwisho wa sala yake au kinyume cha hayo? Ameonelea rai ya mwanzo Mwenye kitabu cha 'Qawaaid al Islaam' kati ya watu wetu, pia jumhuri ya watu wa madhehebu nyenginezo, na wameonelea rai ya pili wingi wa watu wetu na baadhi ya maulama wa madhehebu nyenginezo. Kila moja kati ya makundi mawili hayo limetegemea riwaya. Wa mwanzo wanategemea riwaya isemayo "ما فاتَكُمْ فَأَتِمُّوا" "Kilicho kufutuni timizeni", na wa mwisho wanategemea riwaya isemayo "فاقْضُوا" "lipeni", na riwaya zote mbili ni sahihi. Imamu Nurdin A'Saalimi –Allah amridhie- ana utafiti juu ya maudhui hii ambao ufupisho wake ni kwamba hamna dalili katika riwaya mbili hizo kwa makundi yote mawili, kwasababu "قَضاء" "qadha" katika lugha ya Kiarabu haimaanishi tu kufanya kitu baada ya wakati wake ili kulipa kilichofutu; bali hiyo ni istilahi iliyokuja baadae na kwa hiyo hazichukuliwi kwa maana hiyo aya za Qur'ani na hadithi za Mtume. Linaoneshwa hilo na kauli ya Allah Taala:ﭽ ﭨ ﭩ ﭪ ﭼ الجمعة: ١٠{Na itakapo kwisha Sala…}Na kauli Yake:ﭽ ﮞ ﮟ ﮠ ﭼ البقرة: ٢٠٠{Na mkisha timiza ibada zenu…}Maana ya 'qadha' katika aya mbili hizi siyo kulipa kilichofutu, bali maana yake ni kile kile kinachoitwa 'adaa' (kutekeleza kwa wakati) katika istilahi ya wanausuli na wanazuoni wa fiqhi. Lakini dalili imo katika kauli yake Mtume: "ما فاتَكُمْ" "Kilicho kufutuni…", kwani kukielezea kwa neno kufutu ni dalili ya kwamba anachokisali anayejiunga na imamu baada ya kutanguliwa ndiyo mwisho wa sala yake. Ukikubainikia uzito wa kauli hii hautakutatiza upimaji wa matawi yote ya suala hili kwa msingi huu, kama wajibu wa kusoma sura pamoja na alfaatiha kwa ziliyemfutu rakaa mbili za mwanzo za sala za jahara anapoinuka kuzilipa n.k. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment