Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 5

Nini aseme asiyediriki mwanzo wa sala anapoinuka kukamilisha kilichomfutu katika sala, je atosheke na kusoma alfaatiha na sura au afanye kitu kingine kama iqama au nia?Alipe kila ambacho imamu alimtangulia kwacho katika kisomo, ikiwa ni sala ya kusoma jahara atasoma alhamdu na sura, na ikiwa ni sala ya kusoma siri atasoma alhamdu peke yake, na atafanya yote yaliyomfutu kama ilivotangulia katika jawabu iliyotangulia. Ama iqama hamlazimu kwasababu iqama ya muadhini inawatosheleza wote wanaosali na imamu. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment