Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 2

Wakati gani asome 'istiadha’ asiyediriki mwanzo wa sala ya imamu?Kumekuwa na khilafu kukhusu kusoma 'istiadha’ kwa asiyediriki mwanzo wa sala ya imamu wakati gani huwa? Kuna kauli ni wakati anapoinuka kulipa asichodiriki. Kauli nyengine ni pale anapoanza kusoma Qur’ani na hii ni sahihi zaidi, kwasababu 'istiadha’ imewekwa katika Sharia kwa ajili ya kusoma Qur’ani, kama ilivo wazi katika kauli Yake Taala:ﭽ ﮝ ﮞ ﮟ ﮠ ﮡ ﮢ ﮣ ﮤ ﭼ النحل: ٩٨{Na ukisoma Qur'ani mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani maluuni}Akiakhirisha 'istiadha’ mpaka atakapokuja kulipa asichodiriki kitakuwa kisomo anachosoma na imamu hakijatanguliwa na 'istiadha’. Qutbu al-aimma anaona kuwa imamu humbebea maamuma wajibu wa kusoma 'istiadha’. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment