Ibadhi.com

KUTIMIZA USICHODIRIKI KATIKA SALA: 1

Vipi afanye aliyemdiriki imamu katika sala baada ya takbira ya ihramu? Kama amemdiriki katika rakaa ya pili kwa mfano vipi atimize sala yake?Maamuma akijiunga na imamu wakati imamu ameshamtangulia kwa sehemu katika sala inampasa maamuma alete takbira ya ihramu kisha aanze kusali kuanzia alipofika imamu, kisha amfuate imamu katika sala yake mpaka afike kwenye kutoa salamu. Imamu akitoa salamu yeye hatatoa salamu pamoja naye, bali anainuka bila takbira, akishasimama sawasawa ataanza kusoma alfaatiha na kuleta kila kilichomfutu katika sala kwa imamu. Akifika pale alipomdiriki imamu atakaa chini na kutoa salamu. Kama amemdiriki imamu kwa mfano katika mwanzo wa rakaa ya pili atainuka baada ya imamu kutoa salamu bila takbira, akishasimama sawasawa atasoma kisha atarukuu na kusujudu. Akishamaliza sijda ya pili atainuka kwa takbira, kwasababu muinuko huu ni miongoni mwa yale yaliyomfutu kwa imamu, kisha atakaa bila takbira na atatoa salamu. Na kama imamu alimfutu kwa rakaa moja na kisomo cha rakaa ya pili atainuka baada ya imamu kutoa salamu na atasoma, atarukuu na kusujudu kisha atainuka na atasoma mara ya pili kisha atakaa chini na kutoa salamu, na kama hivi atapima mwenginemo. Na Allah anajua zaidi.

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment