Ibadhi.com

10. KUSTAWI ALLAH MTUKUFU JUU YA ARSHI

Inalazimika kuamini kuwa Allah mtukufu amekalia kiti chake cha enzi (Arshi) nako ni kutawalia mamlaka yake, basi amesema katika Kitabu chake:

الرَّحْمَنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَى

((Mwingi wa rehma juu ya arshi ametawala)) [Taha 5]

Tunaporejea katika Aya za Quraani tukufu zilizokuja kuelezea kukalia Allah mtukufu Arshi yake tunakutia kuwa Aya zote zimekuja kuelezea mamlaka ya Allah mtukufu kwa kuanzisha viumbe vyake, kisha baada ya hapo ndio tunaelezwa kukalia Allah mtukufu kiti chake cha enzi nacho ni Arshi tukufu.

Ametuambia Allah mtukufu:

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ

((Hakika Mola wenu ni Allah aliyeumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akatawala juu ya Arshi......)) [Al Aaraaf 45]

Basi ni wazi kustawi kwa Allah mtukufu juu ya Arshi kusudio lake ni kuwa baada ya kuumba kwake viumbe vyake hakuviwacha nje ya usimamizi wake na mamlaka yake, bali alivitawalia maendesho yake na mambo yake; kwa hiyo kustawi kwa Allah mtukufu juu ya Arshi maana yake ni kutawalia mamlaka yake, na hii ni katika kinaya za lugha na waarabu.

Anatuambia Imamu Atfaish (r.a):

وذلك كناية أُريد بها إلزام المعنى وهو الملك والتصرف ولم يرد بها مع ذلك ظاهر اللفظ

"Na hilo ni kinaya imekusudiwa kwa kinaya hicho ulazima wa maana nayo ni kumiliki na kusimamia, na haijakusudiwa kwa kinaya hicho pamoja na hayo udhahiri wa tamko"

Kwa hiyo inalazimika kumtakasa Allah mtukufu kutokana na sifa ya kukaa kitako juu ya kiumbe chake; kwani Allah mtukufu sio kiwiliwili, wala si mwenye kudhibitiwa kwa mipaka ya sehemu, basi vipi isemwe kuwa yeye amekaa kitako juu ya Arshi hali ya kuwa Arshi ni kiumbe chenye kuzungukwa na malaika na kubebwa, ametakasika Allah mtukufu kutokana na upungufu wote wa kimaumbile. Basi kustawi kwa Allah mtukufu juu ya Arshi yake ni kutawalia kwake mamlaka yake na viumbe vyake, na sio kukaa kitako juu yake.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment