Ibadhi.com

6. INAYOWEZAKANA KUSIFIKA NAYO ALLAH MTUKUFU.

Inawezekana kwa Allah mtukufu kusifika kwa sifa za vitendo vyake vyote kama vile:

  1. kutuma Mitume.
  2. kuteremsha vitabu.
  3. kukiweka kisichokuwepo.
  4. kukiondosha kulichopo.
  5. kukirejesha kilichokuwepo baada ya kukiondosha.

Na anaweza kusifika Allah mtukufu kwa sifa nyengine ambazo kupatikana kwa sifa hizo au kukosekana kwa sifa hizo hakuleti upungufu katika haki yake Allah aliyetukuka.

Kwani hakika ya hayo ni katika mambo yanayofaa kupatikana kutoka kwa Allah mtukufu, na pia inafaa kukosekana kwa mambo hayo katika haki ya Allah mtukufu, na yote hayo ni kwa kutumia hukumu ya akili kabla ya kusikia kupatikana kwa sifa hizo kwa njia ya sheria.

Ama baada ya kusikia sifa hizo kwa njia ya sheria, itakua ni lazima kumsifu Allah mtukufu kwa sifa hizo, kwa sababu haiwezekani yeye awe kinyume na yale aliyotuambia yeye mwenyewe Allah mtukufu.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment